Inter Milan yatwaa ubingwa Ulaya mbele ya Bayern Munich
22 Mei 2010Ni ushidini ambapo umezidi kumyanyua katika chati kocha wa timu hiyo mreno Jose Morinhno.Hii ni mara ya pili kwa Morinho kushinda ubingwa upingwa huo mara ya kwanza akiwa na FC Porto ya Ureno, kabla ya kuchukuliwa na Chelsea ya Uingereza.
Pamoja na kufungwa, lakini Bayern ilionesha mchezo wa hali ya juu ya kumiliki mpitra muda mwingi kuliko wapinzani wao.Arjen Robben alionekana kuwa mwiba katika ngome ya Inter Milan iliyokuwa chini ya beki wa zamani wa Bayern mbrazil Lucio.Lakini ngome ya Bayern ilionekana kutokuwa makini na kutoa mwanya kwa Milito kupachika mabao hayo mawili.
Bayern ilipiga hodi mara nyingi zaidi katika lango la Inter lakini ilikuwa vigumu lango hilo kufunguliwa.Inter walipata nafasi nne ambapo mbili walizitumia kupachika mabao hayo na hivyo kuchukua vikombe vitatu katika msimu mmoja.
Inter Milan wametwaa ubingwa wa ligi ya daraja la kwanza Italia na kombe la chama cha soka nchini humo, kabla ya kutwaa uchampion wa Ulaya.
Jose Morinho amethibitisha umwamba wake katika kufundisha mbinu za kabumbu dimbani na hakuna shaka kuwa ni kocha bora duniani.
Nchini Ujerumani, miji yote ilikuwa kimya, huku washabiki wakirejea nyumbani mapema, na sherehe zilizoandaliwa zilivunjika
Mwandishi.Aboubakary Liongo