1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Interpol yawakamata washukiwa 260 wa utapeli mitandaoni

26 Septemba 2025

Polisi ya kimataifa, Interpol, imesema leo kuwa msako unaoratibiwa na shirika hilo dhidi ya uhalifu wa mtandaoni, umesababisha kukamatwa kwa washukiwa 260 katika nchi 14 za Afrika.

Picha ya matumizi ya mtandao
Matumizi ya mtandaoPicha: Jan Eifert/picture alliance

Katika taarifa, Interpol imesema kwa ujumla ulaghai huo ulilenga zaidi ya wahasiriwa 1,400 ambao walipoteza karibu dola milioni 2.8 milioni.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa huduma za polisi wa shirika hilo la Interpol Cyril Gout, amesema vitengo vya uhalifu wa mtandaoni kote barani Afrika vinaripoti kuongezeka kwa kasi kwa uhalifu unaowezeshwa kidijitali kama vile ulaghai wa kingono na mapenzi.

Ulaghai wa mitandaoni wasababisha madhara kwa waathiriwa

Gout amesema ukuaji wa majukwaa ya mtandaoni umefungua fursa mpya kwa

mitandao ya uhalifu kuwanyonya waathiriwa, na kusababisha hasara ya kifedha na

madhara ya kisaikolojia.

Interpol inasema operesheni hiyo ilifanyika mnamo Julai na Agosti na ililenga ulaghai ambao wahalifu wanajenga mahusiano ya kimapenzi mtandaoni ili kuwatapeli walengwa kwa kitisho cha kuwaharibia sifa kupitia picha chafu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW