1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOC imeipiga marufuku kamati ya Olimpiki ya Urusi

14 Oktoba 2023

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC imesema kwamba imeipiga marufuku kamati ya Olimpiki ya Urusi kushiriki katika michezo kwa kukiuka uadilifu wa eneo la uanachama wa Ukraine.

IOC-Treffen in Indien
Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance/dpa

Hatua ya IOC, ilifikiwa siku ya Alhamisi wakati wa mkutano wa bodi ya watendaji unaoendelea huko Mumbai, baada ya Kamati ya Olimpiki ya Urusi kujumuisha upande wake mashirika ya kikanda kutoka maeneo manne ya Ukraine yaliyotwaliwa tangu uvamizi wa Urusi uanze mnamo 2022.

Soma pia: IOC yakosoa uamuzi wa Ukraine kuwazuia wanamichezo wake

Akizungumzia hatua hiyo, rais wa Shirikisho la Kimataifa la Riadha Sebastian Coe ameitaja kuwa ni uamuzi sahihi na pekee ambao kamati hiyo ilikuwa nao.

Awali shirikisho la kimataifa la riadha lilipiga marufuku wanariadha, makocha na maafisa kutoka Urusi na Belarus tangu Machi mwaka 2022 baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW