IOM: Idadi ya wanaokufa maji kuingia Uarabuni imeongezeka
25 Machi 2026
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja Mataifa la Uhamiaji OIM ambayo imetolewa hii leo Jumatano.
Kila mwaka, maelfu ya wahamiaji kutoka nchi za Ethiopia, Somalia na nchi jirani huhatarisha maisha yao kuvuka bahari ya Shamu wakipitia hasa nchi ya Djibouti kuelekea Yemen.
Ajira ndio kichocheo cha safari za hatari
Matumaini yao ni kupata kazi kama vibarua au watumishi wa nyumbani katika mataifa tajiri ya Ghuba. Akizungumz na shirika la habari la AFP, Tanja Pacifico ambaye ni mkuu wa shirika la OIM nchini Djibouti ameulezea mwaka 2025 kuwa wa hatari zaidi kwani idadi ya watu 922 mara mbili ya mwaka uliotangulia walifariki au kutoweka bila kujulikana waliko walipojaribu kupitia njia hiyo:
Wengi wa waathirika walitokea nchi ya Ethiopia, nchi ya pili kwa idadi ya watu barani Afrika akiwa na zaidi ya watu milioni 130. Hali hii inatokana na mizozo ya ndani ya nchi hiyo na pia umasikini uliokithiri. Tanja amesem kuwa IOM ingali imejitolea kushirikiana na serikali ya Djibouti kuboresha usalama na hadhi ya wale wanaotumia njia hiyo ya uhamiaji ili kuepusha maafa zaidi.
Kukwama kwa wahamiaji wengi nchini Yemen
Wahamiaji wengi wanavuka bahari ya Shamu hujikuta wakiwa wamekwama nchini Yemen, nchi masikini zaidi katika Ghuba la Uarabuni ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa takriban mwongo na baadhi huamua kurudi.
Kuna matumaini kwamba huenda kasi ya ukuaji wa kiuchumi nchini Ethiopia inayoshuhudiwa kwa sasa kwa asili mia 10 itawashawishi wengine kuondokana na fikra ya kuhamia nchi nyingine. Ila kiwango cha mfumko kingali cha juu kwa asili mia 10 kama ilivyobainika mwezi Februari mwaka huu.