1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IPCC:kutoa ripoti ya hali ya joto duniani

Hawa Bihoga
14 Februari 2022

Ripoti hiyo itayoonesha namna ongezeko la joto linavyoharibu maisha ya watu,,azingira ya asili na dunia kwa ujumla wake,inatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Februari.

Berlin | Weltklimarat Konferenz IPCC
Picha: Kriemann/POP-EYE/imago images

Jopo la Umoja wa Mataifa linaloundwa na serikali mbalimbali juu ya mabadiliko ya tabianchi, IPCC, na wanasayansi mahiri duniani, hutoa ripoti tatu kila baada ya miaka 5 hadi 7.

Ripoti ya hivi karibuni ambayo itakuwa tayari mwishoni mwa mezi huu wa Februari inatarajiwa kuelezea namna mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri wanadamu na sayari, kinachotarajiwa baadae, madhara na faida ya hali ya joto duniani.

Mwenyekiti mwenza wa jopo hilo, Debra Robert, ambaye ni mwanasayansi wa mazingira kutoka Afrika Kusini, amesema kwamba ripoti hiyo imejikita katika maeneo saba, ikiangazia namna mabadiliko ya tabianchi yanavyobadili maisha ya watu, kadhalika imeweka msisitizo mkubwa katika miji. 

Soma zaidi: Ripoti ya IPCC: Dunia yashindwa kudhibiti uzalishaji gesi chafu

Hadi sasa bado wanasayansi hawajaweka wazi nini kilichomo kwenye ripoti kwa sababu muhtasari wake bado upo kwenye mjadala mzito kati ya waandaaji na serikali mbalimbali kwa wiki mbili zijazo, ambapo makubaliano yanahitajika ili kupata toleo la mwisho.

Rasimu ambayo ilitolewa kwa majadiliano itabadilishwa kabla ya kutolewa toleo rasmi mnamo Februari 28.

Wanamazingira wasema hali mbaya ya hewa inayoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya dunia katika miaka ya hiki karibuni inaonesha serikali za mataifa zinapaswa kuchukua hatua za dhurura katika kukabiliana na madhara  yanayoongezeka ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kikosi cha kukabiliana na majanga ya moto kikizima moto uliozuka msituni UrusiPicha: Maksim Slutsky/AP/picture alliance

Ripoti ya IPCC inayotarajiwa kutolewa itathibitisha kile kinachojulikana kuhusu matokeo ya wimbi la joto, ukame, mafuriko, vimbunga, majanga ya moto msituni pamoja na kuongezeka kwa asidi kwenye bahari kwenye madhara kwa watu na mifumo ya ikolojia. Alisema Rachel Cleetus kutoka umoja wa wanasayansi.

Soma zaidi:IPCC: Gharika zinatokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi

Waziri wa masuala ya sayansi nchini Ujerumani Bettina Stark-Watzinger  amsema kuna umuhimu kuzishawishi serikali kusaini ripoti itakayotolewa ili kuwe na utashi wa kisiasa ambao utamjumuisha kila mmoja.  

Waziri wa sayansi Ujerumani Bettina Stark-WatzingerPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Mbali na mambo mengine ripoti hiyo pia inatarajiwa kuzungumzia namna mabadiliko ya hali ya hewa yanavyoathiri afya ya akili ya binadamu.

Ripoti hii inayotarahjiwa kutolewa mwisho wa mwezi huu ni ya pili kati ya ripoti nne katika  mfululizo  wa tathmini ya IPCC, ya kwanza ilitolewa mwezi Agosti mwaka uliopita ambayo ilichambua mabadiliko ya hali ya hewa na kutathmini hatua za haraka zitazochukuliwa ili kukabiliana na hali ya ongezeko la joto ambayo ulimwengu unashuhudia hivi sasa.

Chanzo:DPA,AP