1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IRA yasimamisha vita

28 Julai 2005

Dublin:

Wapiganaji wa Jeshi la Jamhuri ya Ireland (IRA) wametangaza rasmi leo kuwa wanasitisha mapigano dhidi ya serikali ya Waingereza katika Ireland ya Kaskazini. Lakini hawakusema chochote kuhusu kuvunjwa kwa jeshi lao kama vile Wapinzani wanavyotaka. Chama kikubwa cha kisiasa cha Waprotestanti katika jimbo hilo, licha ya tangazo hilo, kimesema kuwa muwafaka wa kisiasa utakaorudisha serikali za mitaa katika mkoa huo bado uko mbali. Kimeshikilia kuwa sasa kinataka kuona vitendo badala ya maneno matupu kutoka kwa maadui wake wa Kikatoliki. Hatua hiyo itasababisha kurudiwa kwa mazungumzo yatakayosababisha kupatikana kwa amani ya kudumu katika mkoa huo uliosambaratishwa na vita. Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, amefurahishwa na uamuzi huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW