1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi wa habari wa Iran, Maryam Lotfi atiwa mbaroni

3 Oktoba 2023

Mwandishi wa habari wa Iran, Maryam Lotfi atiwa mbaroni Tehran baada ya kutembelea hospitali kwa lengo la kuripoti hali ya msichana mdogo ambaye alipoteza fahamu wakati akiwa kwenye safari ya treni ya chini ya ardhi

Iran Teheran | Anschlag auf Botschaft Aserbeidschan
Picha: Aziz Karimov/AP/picture alliance

Gazeti analofanyia kazi la Shargh limesema alikuwa ameenda katika Hospitali ya Fajr katika mji mkuu "kutayarisha ripoti ya habari kuhusu hali ya msichana huyo wa miaka 16 aliefikwa na hali ngumu kwenye treni ya chini ya ardhi" siku ya Jumapili.Mazingira ya tukio hilo hayako wazi hadi sasa, huku afisa mkuu akikana "uvumi" wa kutokea ugomvi na wafanyakazi wa treni ya chini ya ardhi.Mwezi Agosti vyombo vya habari vya Iran viliandika kuwa mamlaka ya Irani imewahoji au kuwakamata waandishi wa habari zaidi ya 90 tangu kuzuka kwa wimbi la maandamano nchini kote mwaka jana.