Iran yaendeleza mashambulizi yake katika mataifa ya Ghuba
3 Aprili 2026
Iran imeendeleza mashambulizi yake katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati usiku wa kuamkia leo. Huko nchini Kuwait, shambulizi la Iran limesababisha moto mkubwa katika kiwanda cha kusafisha mafuta.
Marekani na Isreal pia zimefanya mashambulizi ya anga nchini Iran wakati vita hivyo vikikaribia wiki yake ya tano ya mapigano tangu kuanza kwake Februari 28.
Katika hatua nyingine, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kupiga kura leo Ijumaa kuhusu pendekezo la Bahrain ambalo linalenga kujadili hatua mbalimbali za kufuata ili kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz ambao umefungwa na Iran.
Bahrain imependekeza azimio la kuruhusu mataifa kutumia nguvu kuhakikisha usafiri wa kimataifa unaendelea, lakini pendekezo hilo linaonekana kuligawa Baraza la Usalama hata kabla ya kupigiwa kura.