1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haiwataki tena wakimbizi wa Afghanistan

3 Aprili 2004
TEHERAN: Baada ya Afghanistan kuahidiwa misaada ya kifedha ya kimataifa hivi majuzi, serikali ya Iran imewaita warudi makwao wakimbizi wapatao miliyoni 1.5 wa Kiafghani. Kama si hivyo watahamishwa kwa nguvu, liliripoti Shirika la Serikali la Televisheni, IRIB. Kabla ya hapo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran iliwapa wakimbizi hao wa Kiafghani lawama ya kuongezeka ukosefu wa ajira nchini humo. Katika mkutano wa wakopeshaji uliofanywa mjini Berlin wiki iliyopita, Afghanistan iliahidiwa msaada mwengine wa Dollar biliyoni 8.2 wa kukarabati uchumi wake.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW