1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran: Hatuna nia ya kufanya mazungumzo na Marekani

26 Machi 2026

Iran imetupilia mbali mpango wa Marekani wa kusitisha vita huko Mashariki ya Kati huku ikiendeleza mashambulizi zaidi dhidi ya Israel na nchi za Ghuba.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi akizungumza na waandishi wa habari.Picha: Jean Marc Ferré/MAXPPP/picture alliance

Tehran hata hivyo imesema inalipitia tena pendekezo hilo lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema Iran haina nia ya kufanya mazungumzo na wala  haijashiriki katika mazungumzo yoyote ya kukomesha vita.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya White House kusema kuwa rais wa Marekani Donald Trump yuko tayari kuisambaratisha Iran ikiwa itakataa kufikiwa kwa makubaliano. Araghchi ameendelea kuwa kwa sasa Iran imejijingea hadhi ya kutoweza kushambuliwa tena na kwamba maadui zao watahofia kuingia tena katika vita na watu wa Iran.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW