1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Suala muhimu limetatuliwa kuhusu Nagorno-Karabakh

24 Oktoba 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Armenia na Azerbaijan wamekutana Iran, ikiwa ni mazungumzo yao ya kwanza tangu Azerbaijan ifanikiwe kulidhibiti eneo la Nagorno-Karabakh, huku Urusi ikisema seheu kubwa ya mzozo imetatuliwa.

Ilham Aliyev - Nikol Pashinyan - Charles Michel
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel.Picha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Mkutano huo wa baada ya mashambulizi ya Azerbaijan katika eneo linalozozaniwa umefanyika katika kipindi ambacho kimegubikwa na ongezeko la mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amenukuliwa na Shirika la Habari la Urusi, Tass akisema akisema mgogoro wa Armenia na Azerbaijan kwa kiwango kikubwa umetatuliwa. Pande zote mbili zimekubaliana Karabakh ni eneo la Azerbaijan na hilo ndilo lililokuwa kiina cha majadiliano hayo. zaidi amesema "Sasa zimesalia hatua za kiutendaji kwa urejeshaji kamili wa mahusiano, kwanza kabisa maandalizi ya makubaliano ya amani, kuweka mipaka, na uanzishaji wa uhusiano wa usafiri na kiuchumi bila kuingiliwa kwa aina yoyote, kwa kuwa yote hayo yaliridhiwa wakati huo wakati mkutano wa marais wa Urusi, Azerbaijan na Armenia."

Kauli ya Uturuki na Iran kuhusu uhuruwa kimipaka.

Wakimbizi wa Armenia wakiondoka kutoka katika eneo la KarabachPicha: SIRANUSH ADAMYAN/AFP/Getty Images

Mawaziri wa Iran na Uturuki, washirika wakuu wa Azerbaijan, pia walihudhuria mkutano huo. Taarifa ya pamoja inaeleza washiriki walikubali kuheshimu uhuru wa kimipaka katika kila taifa.

Kabla ya mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian, alisema mazungumzo hayo yanawakilisha fursa ya kihistoria katika eneo hilo na kwamba vita vimemalizika, kwa hivyo umewadia sasa wakati wa amani na ushirikiano.

Bila ya kutoa ufafanuzi zaidi aliongeza kwa kusema uwepo wa washiriki kutoka nje ya ukanda huo, si tu kunaongeza matatizo bali kunafanya mambo kuwa magumu zaidi.

Kukosolewa kwa juhudi za amani za Marekani na Umoja wa Ulaya.

Kauli hiyo ilikuwa ikiigusa Marekani na Umoja wa Ulaya, ambao ushiriki wao katika kutafuta makubaliano hayo ya amani kimsingi yameichukiza sana Urusi. Rais wa Iran Ebrahim Raisi, amenukiwa  na vyombo vya habari vya serikali, akisema Tehran iko tayari kusaidia katika kutatua mizozo iliyopo kati ya Azerbaijan na Armenia.

Soma zaidi:Mzozo wa Nagorno-Karabakh wafika mahakama ya haki, ICJ

Eneo la Nagorno-Karabakh kimataifa linatazamwa kama sehemu ya Azerbaijan limekuwa kilidhibitiwa na   Jamii ya Waarmenia waliojitenga tangu kuanguka kwa iliyokua Jumuiya ya Kisovieti katika miaka ya 1990.

Chanzo: RTR

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW