Iran : Idadi rasmi ya waliouawa kwenye maandamano ni 3117
21 Februari 2026
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Araghchi amesema kutimiza ahadi yao ya uwazi kamili
kwa watu wao, Serikali ya Iran tayari imechapisha orodha ya kina ya waathiriwa wote 3117 wa kile alichokiita operesheni ya hivi karibuni ya kigaidi, wakiwemo maafisa wapatao 200.
Amesema yeyote anayetilia mashaka takwimu hizo aweke wazi ushahidi. Hata hivyo hakusema kilichochochea chapisho hilo.
Hapo jana, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba watu 32,000 waliuawa katika muda mfupi nchini Iran, bila kutaja chanzo cha idadi hiyo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu (HRANA) lenye makao yake nchini Marekani, zaidi ya watu 7,000 waliuawa katika msako mkali wa mamlaka ya Iran dhidi ya maandamano ya kuipinga serikali yaliyochochewa na hali mbaya ya kiuchumi.