1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran inataka kumuua Trump - Idara ya Ujasusi Marekani

25 Septemba 2024

Idara ya Ujasusi ya Marekani imemuonya mgombea urais kwa tiketi ya Republican, Donald Trump, juu ya kile inachodai ni kitisho cha kweli na cha wazi kutoka Iran inayotaka kumuua.

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump.
Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump.Picha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Timu ya kampeni ya mgombea huyo ilisema kwenye taarifa yake ya jana kwamba Ofisi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ilimpa taarifa kwamba kumekuwa na juhudi za wazi za kumuua kutoka Iran, kwa lengo la kuihujumu Marekani na kupandikiza machafuko.

Kwa mujibu wa timu hiyo, idara ya ujasusi inaamini kumekuwa matukio ya mashambulizi dhidi ya Trump katika miezi ya karibuni na kwamba imeimarisha ulinzi kwa bilionea huyo anayetaka kurejea madarakani kupitia uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu. Iran inakanusha vikali tuhuma hizo.

Soma zaidi: Viongozi ulimwenguni walaani shambulio dhidi ya Donald Trump

Marekani inafanya uchaguzi wake mkuu tarehe 5 Novemba, ambapo hadi sasa utafiti wa maoni ya wapigakura yanaonesha kuwa Trump na hasimu wake wa Democrat, Kamala Harris, wanachuana vikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW