JamiiAsia
Iran kuendelea na hukumu ya kifo kwa daktari raia wa Sweden
25 Mei 2022Matangazo
Msemaji wa mahakama, Masoud Setayeshi amenukuliwa akisema "Hukumu hiyo ni ya kisheria, isipokuwa ni jukumu la upande wa mashtaka pekee ndio wenye kupaswa kuamua muda wa kutekelezwa."
Setayeshi amefutilia mbali uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia kama vile mabadilishano ya wafungwa.
Daktari huyo ambaye pia ni mhadhiri alitiwa mbaroni 2016 wakati alipowasili nchini Iran, kwa tuhuma za kulifanyia kazi shirika la kijasusi la Israel Mossad. Mahakama ya walinzi wa mapinduzi ilimuhukumu kifo.
Hukumu hiyo ilithibitishwa na mahakama ya juu kabisa ya Iran mnamo 2017 na kukosolewa na wanadiplomasia. Mwaka mmoja baadaye akapata uraia wa Sweden. Iran na Israel zimekuwa katika uhasama kwa zaidi ya miaka 40.