1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran kufanya mazungumzo ya Nyuklia na mataifa ya Ulaya

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Iran imetangaza kuwa itafanya mazungumzo ya nyuklia na nchi tatu za Ulaya — Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza — wiki ijayo mjini Geneva.

Serikali ya Iran kufanya mazungumzo ya Nyuklia na mataifa matatu ya Ulaya mjini Geneva
Serikali ya Iran kufanya mazungumzo ya Nyuklia na mataifa matatu ya Ulaya mjini GenevaPicha: Lisi Niesner/REUTERS

Iran imetangaza kuwa itafanya mazungumzo ya nyuklia na nchi tatu za Ulaya — Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza — wiki ijayo mjini Geneva.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 29 na yatahusu mzozo wa mpango wa nyuklia wa Iran, kufuatia azimio lililopitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti wa nyuklia dhidi ya Iran. Iran ilijibu azimio hilo kwa hatua kama vile kuwasha vinu vipya na vya kisasa vya urutubishaji wa urani.

Serikali ya Rais Masoud Pezeshkian inatafuta suluhu ya mkwamo wa nyuklia kabla ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, Januari.