Iran: Marekani kuachia mali iliyofungiwa Qatar
11 Aprili 2026
Chanzo hicho kilichozungumza kwa sharti la kutotajwa jina kutokana na suala hilo kuwa nyeti, kimepongeza hatua hiyo na kuitaja kuwa ishara ya uzito wa kufikia makubaliano na Marekani katika mazungumzo mjini Islamabad nchini Pakistan.
Pia kimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba kuachia mali hiyo kulihusishwa moja kwa moja na kuhakikisha usalama wa safari za meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz suala linalotarajiwa kuwa la kipaombele wakati wa mazungumzo hayo.
Hata hivyo, Marekani haijatoa tamko kuhusu suala hilo.
Tayari ujumbe wa Marekani unaoongozwa na naibu rais JD Vance umewasili Pakistan kwa mazungumzohayo na maafisa wa Iran ambao pia waliwasili mapema leo wakiongozwa na spika wa bunge Mohammad Bagher Qalibaf, yanayolenga kutafuta suluhisho la kudumu la vita Mashariki ya Kati.