1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Iran: Mashambulizi dhidi ya Syria huenda yakachochea visasi

31 Agosti 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amirab-dollahian amelaani shambulio la anga la Israel kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Syria ulioko Aleppo, akisema mashambulizi kama hayo huenda yakachochea visasi.

Syrien| Flughafen Aleppo | Archivbild
Picha: Uncredited/SANA/AP/dpa/picture alliance

Amirab-dollahian ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika mji mkuu wa Syria, Damascus ambapo anaanza ziara ya siku mbili.

Mnamo siku ya Jumatatu, shambulio la anga la Israel liliharibu uwanja wa ndege wa Aleppo na kusababisha barabara ya kutua na kupaa kwa ndege kutofanya kazi. 

Soma pia:Iran, Iraq zakubaliana kupambana na 'magaidi' Kurdistan

Uwanja huo wa ndege umelengwa kwa mashambulizi kadhaa mwaka huu, ikiwemo mashambulizi mawili mwezi Machi yaliokwamisha kabisa oparesheni kwenye uwanja huo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Israel imefanya mashambulizi yaliyolenga vikosi vya jeshi la Syria au makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Iran japo ni nadra kwa Israel yenyewe kuthibitisha kuhusika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW