1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran na Bahrain zaridhia mazungumzo ya kurejesha mahusiano

24 Juni 2024

Iran na Bahrain wamekubaliana kuanzisha mazungumzo ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia yaliyovurugika kwa karibu miaka minane.

Iran | Bahrain
Mawaziriwa mambo ya kigeni wa Iran na Bahrain walipokutana kwa mazungumzo mjini Tehran mnamo Juni 23, 2024.Picha: irna

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema, kaimu Waziri wa Mambo ya Nje Ali Bagheri jana Jumapili alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Abdullatif bin Rashid al-Zayani pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa nchi za Asia, ACD mjini Tehran.

Kwenye mkutano wao walikubaliana kuanzisha mkakati muhimu wa kuanza mazungumzo ya kusaka namna ya kurejesha uhusiano wa kisiasa.

Bahrain ilisitisha uhusiano na Iran mwaka 2016 baada ya ujumbe wa kidiplomasia wa Riyadh nchini Irankushambuliwa na waandamanaji waliokuwa wakipinga hatua ya Saudi Arabia ya kumuua ulamaa maarufu wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia.