1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran na Marekani zashambuliana kwa droni

28 Mei 2026

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la Iran limeishambulia kambi ya jeshi la anga la Marekani baada Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya operesheni ya droni za Iran karibu na Mlango Bahari wa Hormuz.

Ndege ya kivita ya Marekani ikipaa kutoka kwenye manowari ya Marekani ya USS Abraham Lincoln
Jeshi la lilikishambulia kituo cha operesheni katika mji wa bandari wa Bandar Abbas nchini IranPicha: US Central Command/dpa/picture alliance

Hayo yalijiri saa chache baada ya Rais Donald Trumpkupinga ripoti kwamba anakaribia kufikia makubaliano na Tehran. Afisa huyo wa Marekani, ambaye aliomba kutotajwa jina lake ili kuzungumza waziwazi kuhusu operesheni za kijeshi, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba jeshi lilidungua ndege nne zisizo na rubani za Iran na kukipiga kituo cha operesheni katika mji wa bandari wa Bandar Abbas ambacho kilikuwa karibu kurusha droni ya tano.

Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kimesema kiliilenga kambi ya Marekani kujibu kile kilichoelezea kama shambulio la mapema asubuhi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Bandar Abbas. Kuwait - ambayo ina kambi kubwa ya Marekani - ilisema iliyajibu mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani bila kusema mashambulizi hayo yalitoka wapi.

Trump amesema mara kwa mara kwamba vita hivyo vinakarabia kumalizika lakini aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa baraza la mawaziri Jumatano kwamba bado hajaridhika na mpango wa Iran na Marekani haijadili kuhusu kupunguza vikwazo dhidi yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW