1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran na Pakistan zaombwa kujizuia kufuatia shambulio la anga

17 Januari 2024

China imezitolea mwito Pakistan na Iran wa kujizuia baada ya Pakistan kusema, Iran imefanya shambulio la anga kwenye ardhi yake lililosababisha vifo vya watoto wawili.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning Picha: Kyodo/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa, amezihimizia nchi hizo mbili jirani kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kusababisha kuongezeka kwa mvutano kati yao.

Iran yafanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo Pakistan

Pakistan imelaani shambulio hilo la anga, karibu na mpaka wake na Iran jana jioni, na kusema tukio hilo halikubaliki na kwamba hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Iran na Pakistan ni washirika wa karibu wa China na pia ni wanachama wa shirika la ushirikiano la Shanghai.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW