Iran: Umoja wa Ulaya usuluhishe mzozo wa nyuklia
2 Februari 2021Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha CNN Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad Zarif amesema kuwa mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Joseph Borell anaweza kuratibu hatua zinazohitajika kwa ajili ya ya Marekani na Iran kurejea kwenye mkataba wa nyuklia.
Katika mahojiano hayo, alipoulizwa ikiwa kurejea kwenye makubaliano ya nyuklia kutahitaji kwanza Iran na Marekani kukidhi vigezo, Zarif alisema hatua muhimu zinaweza kuchukuliwa kwa wakati huohuo ama kwa mpangilio maalumu. Kwa mujibu wa Zarif, hatua hii huenda ikaungwa mkono na Borell ambaye sehemu ya wajibu wake ni kuratibu kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya silaha za nyuklia, kamisheni inayoundwa na mataifa sita yakiwemo Uingereza, China, Ufaransa, Urusi na Marekani.
Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Iran ameonesha matumaini kuwa huenda nchi yake ikaachana na uzalishaji kwa kiwango kikubwa wa madini ya Urani ndani ya muda mfupi ikiwa Marekani itaondoa vikwazo ilivyoiwekea wakati wa utawala wa rais Donald Trump na kurejea kwenye makubaliano ya kimataifa ya nyuklia yam waka 2015. "Napaswa kusisitiza kwamba Merekani ndiyo ilijitoa kutoka makubaliano na kuvunja ahadi zake. Sasa ni Marekani inayopaswa kujrejea kwenye makubaliano na kutimiza ahadi. Marekani itakapofanya hivyo na tukaona faida ya hatua hizo, tutatekeleza kikamilifu wajibu wetu kama ilivyotangazwa na uongozi wa juu wa Jamhuri ya Kiislamu."
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken alisema kuwa taifa lake litarejea kwenye makubaliano, iwapo Iran itazingatia masharti yaliyoainishwa kwenye mkataba huo. Awali rais wa Iran Hassan Rowhani aliitaka Marekani iichukue hatua ya kwanza katika kuutatua mzozo huo kwandi ndiyo iliyojitoa katika mkataba huo.
Soma pia: Iran kurutubisha madini ya Uranium kwa asilimia 20
Chini ya makubaliano hayo, Iran ilikubali kupungza uzalishaj wa silaha za nyuklia kwa sharti la Marekani kuiondolea vikwazo vya kiuchumi, Rais aliyemaliza mud wake Donald Trump alijiondoa kwenye maakubaliano hayo mnamo mwaka 2018. Rais wa sasa wa Marekani Joe Biden amesisitiza kuwa kama Iran itazingatia masharti, nchi yake itarejea kwenye makubaliano hayo.
Soma pia: Mataifa kadha yajaribu kuunusuru mkataba wa nyuklia na Iran
Wakati huohuo, Iran jana jumatatui litangaza kuwa imefanikiwa kufanyia majaribio roketi ya kubeba satelaiti iitwayo Zuljanah iliyopewa jina la farasi wa mtume Mohamad, Imam Hussein. kwa mujibu wa wizara ya ulizni ya Iran, roketi hiyo ina uwezo wa kubeba zaidi ya kilo 220 angani na kupaa angani umbali wa kilometa 500. Iran inasema, satelaiti zake hutumika kutoa taarifa kuhusu hali ya hewa, majanga ya asili na kilimo na si kwa ajili ya matumizi ya kijeshi.
afp, reuters, ap