1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran: Waandamanaji waadhimisha mwaka mmoja wa ukandamizaji

30 Septemba 2023

Waandamanaji wamekabiliana na vikosi vya usalama vya Iran katika eneo la kusini mashariki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya ukandamizaji wa vikosi vya usalama iliyopewa jina la "Ijumaa ya Umwagaji Damu."

Maandamano mjini Zahedan
Maandamano mjini ZahedanPicha: UGC

Vidio zilizochapishwa kwenye mtandao wa X na shirika la kutetea haki za binadamu la Iran - IHR, zimeonyesha waandamanaji wakikabiliana na vikosi vya usalama mjini Zahedan, mji mkuu wa mkoa wa kusini mashariki wa Sistan-Baluchistan.

Mashirika ya haki za binadamu ya IHR na Hal Vash yamesema takriban watu 23 wamejeruhiwa. Shirika la habari la Reuters hata hivyo halikuweza kuthibitisha ripoti za majeruhi hao au uhalisia wa vidio zilizochapishwa mtandaoni.

Shirika la Amnesty International limeeleza kuwa, mnamo Septemba 30 mwaka jana, vikosi vya usalama vya Iran viliua takriban watu 66.

Mamlaka iliwatuhumu waandamanaji, waliokasirishwa na madai ya kubakwa kwa msichana kutoka jamii ya walio wachache ya Baluch na kamanda wa polisi, kwa kuchochea ghasia hizo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW