1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Iran wapigakura duru ya pili kumchaguwa rais

5 Julai 2024

Wapigakura nchini Iran wanamiminika vituoni kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais kumchaguwa mrithi wa Marehemu Ibrahim Raisii aliyefariki dunia kwa ajali ya ndege mwezi Mei.

Iran I 2024
Wagombea urais wa Iran, Saeed Jalili (kushoto) na Masoud Pezeshkian.Picha: Iranian State Tv/ZUMAPRESS/picture alliance

Uchaguzi wa leo ni baina ya mwanamageuzi Masoud Pezekshian na mhafidhina Saeed Jalili.

Kwenye duru ya kwanza wiki iliyopita, Pezekshian alipata asilimia 42, huku Jalili akimfuatia kwa asilimia 39 ya kura.

Soma zaidi: 

Juzi Jumatano, kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, aliwatolea wito wananchi kujitokeza kwa wingi vituoni, baada ya duru ya kwanza kushuhudia asilimia 41 tu ya wapigakura halali.

Pezekshian, ambaye ni daktari bingwa wa moyo na pia mbunge wa mji wa kaskazini magharibi wa Tabriz tangu  mwaka 2008, anaungwa mkono na marais wawili wa zamani, Mohammad Khatami na Hassan Rouhani, wote wanamageuzi. 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW