1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Iran yaapa kushambulia mabenki ya Israel na Marekani

11 Machi 2026

Jeshi la Iran limeapa kuendelea kushambulia miundombinu ya kiuchumi ya Marekani na Israel katika eneo zima la Mashariki ya Kati. Hayo yanajiri wakati Mojtaba Khamenei, akiwa bado hajasema lolote kuhusiana na vita hivyo.

Libanon Beirut 2026 | Feuerwehr inspiziert ausgebrannte Wohnung nach israelischem Luftangriff
Iran na Israel zimeendelea kushambuliana kwa makombora na droni huku Tehran ikiongeza mbinyo wake kwenye sekta ya mafuta kwenye eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati.Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Iran imesema mashambulizi yake yatalenga mabenki ya Israel na Iran baada ya benki yake kuu kushambuliwa na mahasimu wake hao.

Kamanda anayeongoza operesheni ya vita Khatam Al-Anbiya, amesema maadui wa taifa la Iran wameipa uhuru wa moja kwa moja nchi hiyo kushambulia maeneo hayo ya Israel na Marekani

Kulingana na mashirika ya habari ya Iran, shambulizi dhidi ya benki kuu ya Iran lililotokea usiku wa kuamkia leo limesababisha mauaji ya wafanyakazi wake kadhaa.

Hayo yanajiri wakati Kiongozi Mkuu mpya wa Iran Mojtaba Khamenei, akiwa bado hajasema lolote kuhusiana na vita vinavyoendelea siku tatu tangu alipochaguliwa kuchukua nafasi hiyo, baada ya baba yake Ayatollah Ali Khamenei kuuawa Februari 28.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW