1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran: Ushirikiano wetu na IAEA hauna tena umuhimu

5 Oktoba 2025

Mwanadiplomasia mkuu wa Iran amesema ushirikiano kati ya Tehran na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu matumizi ya nishati ya nyuklia (IAEA) hauna tena umuhimu baada ya nchi hiyo kuwekewa upya vikwazo vya kimataifa.

Tehran 2025 | Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi
Abbas Araghchi - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Picha: Iranian Foreign Ministry/ZUMA Press Wire/IMAGO

Abbas Araghchi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema makubaliano kati ya Iran na  IAEA  ya mwezi Septemba huko Cairo hayana tena nafasi.

Tehran ilimlaumu mkuu wa shirika hilo Rafael Grossi kwa kutoa taarifa zilizokinzana ambazo wanadai zilipelekea mashambulizi ya Israel na Marekani mwezi Juni mwaka huu.

Hivi majuzi, mataifa makubwa ya magharibi yalichukua uamuzi wa kuiwekea tena vikwazo Iran  yakitaja kuwa nchi hiyo imeshindwa kutoa ushirikiano kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW