Iran yaelezea hofu makabiliano ya Israel na Hezbollah
24 Septemba 2024Iran leo imeelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon. Wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Tehran, msemaji wa serikali ya Iran Fatemeh Mohajerani, amesema nchi hiyo inalaani vikali mashambulizi hayo na kutaka muingilio wa haraka wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Tuna wasiwasi kuhusu hali ya kurudiwa kwa majanga kama yale yaliyotokea Gaza na Rafah, na kwa hivyo, tunataka uingiliaji wa haraka wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."
Israel na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran, leo zilikabiliana tena katika mashambulizi siku moja baada ya shambulizi kubwa la Israel kusababisha vifo vya takriban watu 500, maelfu kukimbia makazi yao kusini mwa Lebanon na kuziacha pande hizo mbili kwenye ukingo wa vita kamili.