1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaendeleza mashambulizi dhidi ya Israel na majirani

24 Machi 2026

Iran imeendelea na mashambulizi yake dhidi ya Israel na nchi za Kiarabu za Ghuba siku ya Jumanne.

Israel Tel Aviv 2026 | Jeshi la zima moto lazima moto kwenye jengo lililoharibiwa na shambulizi la makombora la Iran
Wazima Moto wakizima moto baada ya shambulizi la Iran lililoharibu jengo mnamo Machi 24, 2026 mjini Tel Aviv nchini Israel. Picha: Erik Marmor/Getty Images

Iran imeendelea na mashambulizi yake dhidi ya Israel na nchi za Kiarabu za Ghuba siku ya Jumanne, huku kombora moja likishambulia barabara katikati ya mji wa Tel Aviv nchini Israel.

Mwandishi wa shirika la Habari la AP aliyekuwa katika eneo la shambulio la makombora ya Iran dhidi ya Tel Aviv aliona shimo kubwa ardhini mapema leo kutokana na shambulio hilo.

Afisa wa idara ya zima moto na uokoaji wa Israel katika eneo la shambulio Avi Gabbay amesema "kwa bahati nzuri, hakukuwa na vifo wala majeruhi vilivyopatikana katika majengo. Kwa ujumla, ilikuwa ushirikiano bora kabisa pamoja na vikosi vyote washirika, ikiwa ni pamoja na polisi.”

Haya yanajiri licha ya rais wa MarekaniDonald Trump kusema jana kwamba Marekani iko katika mazungumzo na Jamhuri hiyo ya Kiislamu kumaliza vita ambavyo vimetanuka kote Mashariki ya Kati.

Trump pia alisitisha kwa siku tano tarehe ya mwisho kwa Irankufungua njia ya mlango wa Bahari Hormuz kwa usafirishaji wa meli la sivyo vituo vyake vya umeme vishambuliwe. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW