1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yafanya luteka katika visiwa vya Uajemi

2 Agosti 2023

Kikosi cha ulinzi wa mapinduzi ya Iran IRGC kimefanya luteka za kushtukiza za kijeshi kwenye visiwa vinavyozozaniwa vya Ghuba ya Uajemi, katika wakati ambapo idadi ya wanajeshi wa Marekani imeongezeka katika eneo hilo.

Iran Soldaten
Picha: Iranian Army/WANA/REUTERS

Shirika la habari la Iran, IRNA limeripoti kuwa luteka hizo za kijeshi zimefanyika zaidi katika kisiwa cha Abu Musa, japo kikosi hicho cha ulinzi wa mapinduzi ya Iran kimeonekana pia kwenye kisiwa cha Tunb.Meli, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na vitengo vya kurusha makombora ndivyo vilivyoshiriki katika luteka hizo za jeshi.Hata hivyo, Iran haikutoa sababu za kufanyika kwa luteka hizo, japo luteka kama hizo zimewahi kufanyika katika miaka ya nyuma.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW