1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yaionya Marekani kwamba iko tayari kwa lolote

22 Januari 2026

Mvutano kati ya Iran na Marekani unaendelea kupamba moto baada ya Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC kutoa onyo kali kwa Washington kufuatia wimbi la maandamano makubwa nchini Iran.

Iran | General Ahmad Vahidi | IRGC
Jenerali Ahmad Vahidi baada ya kuteuliwa kuwa naibu kamanda wa IRGCPicha: Irna.ir

Kamanda huyo Mohammad Pakpour amesema kuwa jeshi lake "limeweka kidole kwenye kitufe cha kufyatua risasi," kauli inayodhihirisha kiwango cha tahadhari ambacho Iran inadai kujihami nacho wakati huu wa sintofahamu ya kisiasa na kiusalama.

Kauli hiyo ameitoa wakati Rais wa Marekani Donald Trump akionyesha ishara za uwezekano wa mazungumzo, akisema kuwa Iran "inaonekana kuwa tayari kuzungumza."

Hata hivyo, licha ya sauti za kidiplomasia, mazingira ya mvutano bado ni makubwa, yakichochewa na matukio ya hivi karibuni ya maandamano yaliyokumbwa na ukandamizaji mkali ndani ya Iran.

Katika hotuba yake, Pakpour amesisitiza kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu "limejiandaa kuliko wakati mwingine wowote," likiwa tayari kutekeleza maagizo ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Alimtaja Khamenei kama kiongozi "mpendwa kuliko maisha yao wenyewe," akionyesha kiwango cha utiifu na uaminifu wa jeshi hilo kwa uongozi wa juu wa Iran.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW