Iran yakamata meli ya kigeni iliyobeba mafuta 'ya magendo'
28 Januari 2024Shirika la habari la Tasnim la Iran limeripoti kuwa meli hiyo "ilikamatwa kwa mujibu wa amri ya mahakama," likimnukuu kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Haidar Honaryan.
Soma pia: Iran yaikamata meli ya mafuta katika Ghuba ya Oman
Honaryan amesema wafanyakazi kumi na wanne wa meli hiyo pia walikamatwa, na kuongeza kwamba walikuwa raia wa "nchi mbili za Asia", bila ya kuzitaja kwa majina.
Iran, mzalishaji mkuu wa mafuta, ni miongoni mwa mataifa yenye bei nafuu zaidi ya mafuta ya petroli duniani, jambo linalochangia vitendo vya usafirishaji haramu wa mafuta.
Mwezi Septemba, Iran ilikamata meli mbili za mafuta zilizokuwa zikipeperusha bendera za Panama na Tanzania na kuwakamata wafanyakazi wao kwa madai ya kusafirisha mafuta ya magendo katika eneo la Ghuba.