1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yakanusha kuongeza kurutubisha madini ya urani

20 Februari 2023

Iran imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba imeongeza kurutubisha madini ya urani kama sehemu ya mpango wake wa nyuklia wenye utata.

Uran l Atom-Symbol und die iranische Flagge
Picha: Dado Ruvic/REUTERS

Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia, IAEA, lilisema jana kuwa linafanya mazungumzo na Iran, baada ya shirika la habari la Bloomberg kuripoti kuwa wakaguzi wa IAEA wiki iliyopita waligundua urani iliyorutubishwa kwa asilimia 84.

Msemaji wa IAEA nchini Iran, Behruz Kamalvandi, amezielezea taarifa hizo kama kashfa na zenye kupotosha ukweli.

Mwanadiplomasia kutoka nje ya Iran amelithibitishia shirika la habari la Ufaransa, AFP, kwamba takwimu zilizoripotiwa na Bloomberg ni za kweli.

Awali, Umoja wa Ulaya ulisema kwamba mpango wa Iran wa kurutubisha uranium utachukuliwa kama kujiondoa kwake kwenye makubaliano ya kinyuklia.