Iran yakanusha kurusha makombora Uturuki
31 Machi 2026
Haya yanajiri huku Iran kupitia waziri wake wa mambo ya kigeni Abbas Araghchi ikipuuzilia mbali ripoti kuwa nchi hiyo ilirusha makombora kuelekea Uturuki na kudai kuwa italichunguza tukio hilo.
Katika mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya kigeni wa Uturuki Hakan Fidan, Araghchi amesema Iran iko tayari kwa ushirikiano wa pamoja kuchunguza tukio hilo.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump leo ameelezea kufadhaishwa na washirika wake ambao hawajaonesha nia ya kuisaidia Marekani katika vita dhidi ya Iran.
Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amewaambia washirika hao kuwa "waende kutafuta mafuta yao wenyewe."
Naye waziri wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amewaambiwa waandishi wa habari kuwa Marekani inafahamu kile inachofanya China na Urusi kuisaidia Iran katika vita na inakabiliana na hilo.
Hegseth amesema siku chache zijazo zitakuwa muhimu kufahamu mwelekeo wa vita hivyo vya Mashariki ya Kati.