1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakanusha madai ya kumuua Trump

9 Novemba 2024

Iran imekanusha kwamba ilikuwa na mipango ya kumuua rais mteule wa Marekani, Donald Trump, baada ya madai hayo kutolewa hapo jana na wizara ya sheria ya Marekani.

Esmail Baghaei
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Iran, Esmaeil Baghaei,Picha: irna.ir

Taarifa ya msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Iran, Esmaeil Baghaei, imesema madai hayo hayana msingi wowote. 

Baghaei amesema Marekani imeshawahi kutoa madai kama hayo na kurejelea tena kauli hiyo, kunaonyesha wazi ni ya kupangwa na iliyo na nia mbaya ya kusambaratisha zaidi mahusiano kati ya Iran na Marekani. 

Iran yalaani vikwazo vipya dhidi yake

Wiki kadhaa iliyopita timu ya kampeni ya Trump ilisema ilipewa taarifa na shirika la ujasusi kuhusu kitisho cha kweli kutoka Iran cha kumuua rais huyo mteule.