1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yakanusha tuhuma za kuhusika na mauaji ya wanajeshi

29 Januari 2024

Iran leo imekanusha tuhuma zinazotolewa na Marekani zinazoihusisha nchi hiyo na mashambulizi yaliyouwa wanajeshi watatu wa Marekani Kaskazini mwa Jordan.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Picha: Office of the Iranian Supreme Leader/AP/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Nasser Kanaani amesema madai hayo hayana msingi.

Kanaani amesema muendelezo wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Syria na Iraq pamoja na vita katika Ukanda wa Gaza ni masuala yatakayozidisha hali ya kuendelea kwa ukosefu wa uthabiti katika kanda hiyo.

Kanaani ameongeza kusema Jamhuri ya Kiislamu haitowi maelekezo kwa kile alichokiita ''makundi ya harakati''.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW