Iran yakanusha ujenzi wa kituo cha siri cha nyuklia
16 Novemba 2025
Hayo yamesema leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na kuongeza kuwa hakuna urutubishaji wowote unaoendelea kwa sasa, baada ya vituo kuharibiwa katika uchokozi wa siku 12 wa Israel na Marekani ulipolekea vita baina yao ambavyo pia vilivuruga mazungumzo ya nyuklia kati ya Tehran na Washington.
Kauli hii ya Iran imetolewa baada ya vyombo vya habari nchini Marekani kuripoti kwamba Iran inaharakisha ujenzi wa kituo cha siri chini ardhi karibu na Natanz.
Aidha Iran imetishia kukagua upya uhusiano wake na shirika la IAEA endapo azimio la kuipinga litapitishwa. Vita vya Juni viliharibu miundombinu na kusitisha mazungumzo ya nyuklia na Marekani, huku Iran ikisisitiza juu ya haki yake ya urutubishwaji wa madini ya urani "kwa matumizi chanya."