SiasaIran
Iran yakosoa mipango ya kurekebisha uhusiano na Israel
1 Mei 2024Matangazo
Matamshi ya Khamenei yamekuja wakati waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken aliposema nchi yake inakaribia kuwa tayari na mpango wa usalama kwa Saudi Arabia iwapo itarekebisha mahusiano yake na Israel.
Taifa hilo la kiarabu limekuwa katika mazungumzo ya kurekebisha mahusiano hayo, lakini yakasimamishwa kwa muda wakati vita kati ya Israel na Hamas vilipoanza. Wasiwasi wa kikanda umeongezeka tangu kuanza kwa vita hivyo vilivyoingiliwa pia na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Syria, Lebanon, Iraq na Yemen.
Iran inaliunga mkono kundi la Hamas lakini imekanusha kuhusika moja kwa moja na shambulizi la kundi hilo kusini mwa Israel.