1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakosoa vikali vikwazo vipya vya Marekani

21 Agosti 2026

Iran imekosoa vikali vikwazo vipya vya Marekani, ambavyo Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, amevieleza kuwa ni “vikwazo vikali zaidi kuwahi kuiwekea Iran.”

Iran Tehran 2024 | Mohammad Baqer Qalibaf
Qalibaf ameituhumu Marekani na Israel kwa kuendesha "vita vya kiuchumi na kisaikolojia.” Picha: Shadati/Xinhua/dpa/picture alliance

Spika wa Bunge la Iran, Mohammed Baqer Qalibaf, amesema Tehran lazima ipange mikakati ya kushinda kile alichokiita vikwazo visivyo vya haki, akisisitiza kuwa maendeleo ya kiuchumi na kiusalama vinategemeana.

Qalibaf ameituhumu Marekani na Israel kwa kuendesha "vita vya kiuchumi na kisaikolojia,” baada ya kutambua kuwa hawawezi kushinda vita ya moja kwa moja dhidi ya Iran na Iraq. Ameitaka Baghdad kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kutumia sarafu za kitaifa kupunguza utegemezi wa dola.

Wakati huo huo, China imesema vikwazo na shinikizo la Marekani havitamaliza mgogoro wa Mashariki ya Kati, ikisisitiza suluhu ya kisiasa na kidiplomasia. Beijing imekosoa vikwazo vya upande mmoja visivyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku Washington ikitaka China ijiunge na kampeni ya kuibana Iran kiuchumi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW