1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakubali kurudi mezani

Admin.WagnerD9 Aprili 2012

Iran imeonyesha dalili za kulegeza msimamo kuhusiana na mpango wake wa nyuklia wakati ikijiandaa kukutana na mataifa yenye nguvu kiuchumi, mjini Istanbul uturuki wiki hii.

Picha ya setilaiti ikionyesha urutubishaji wa madini ya uranium nchini Iran
Picha ya setilaiti ikionyesha urutubishaji wa madini ya uranium nchini IranPicha: AP

Mkuu wa nyuklia wa Iran Fereioun Abbas amesema Iran inaweza kusitisha urutubishaji wa madini ya Uranium lakini itaendelea na mpango wake wa kuzalisha mafuta ya nyuklia kwa ajili ya umeme.

Pendekezo hili lililotolewa na Iran siku ya Jumapili linalenga kuzungumzia moja kwa moja, suala muhimu katika mazungumzo yalipangwa kuanza siku ya Ijumaa kati ya Iran na Mataifa matano wanachama wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, lakini Irani imesema haitakubali mashgarti yoyote yatakayotolewa kwake kabla ya mkutano huo.

Pendekezo latiliwa shaka
Lakini pendekezo hili linaweza lisiishwaishi Marekani na nchi nyingine zinazoishtumu Iran kwa kuzalisha na kuweka uranium ambayo imerutubishwa hadi kufikia asilimia 20 kama itaendelea kubaki mikoni mwake. Wataalam wanasema nishati hii inaweza kuongezwa nguvu na kuzalisha silaha za nyuklia ndani ya miezi michache tu.

Abbas alisema Iran inaweza kusitisha uzalishaji wa Uranium iliyorutubishwa kwa kiwango hiki cha asilimia 20, na kutumia hii iliyo nayo sasa hivi kwa ajili ya kinu cha utafiti, huku ikiendelea kurutubisha nyingine kwa kiwango cha chini kwa ajili ya kuzaalishia umeme.

Kiini cha mgogoro
Urutubishaji wa uranium ndiyo kiini cha mgogoro kati ya irani na Mataifa ya magharibi ambayo yanahofu kuwa nchi hii inataka kuzaalisha silaha za atomik, lakini utawala mjini Tehran unakanusha vikali shutuma hizi, na kusistiza kuwa mpango wake ni wa amani.

Rais Mahmood Ahmadnajad akitembelea kituo cha kurutubisha uranium cha ´NantazPicha: AP

Uranium inapaswa kurutubishwa kwa kiwango cha asilimia 90 ili kuweza kutengeneza bomu la nyuklia lakini nchi za magahrabi zinasema kiwango ilichofikia Iran cha asilimia 20 kinaipeleka karibu kabisaa na utengenezaji wa bomu hilo la nyuklia.

Abbas alisema uzalishaji wa uraniuma iliyorutubishwa kwa zaidi ya asilimia 20 si moja ya mipnago ya muda mrefu ya taifa hilo la kiislam ambalo anasema linahitaji urutubishaji wa kiwango hicho cha asilimia 20 kwa ajili ya utafiti tu na kusisitiza kuwa hawahitaji kurutubisha zaidi ya hapo.

Alisema urutubishaji huu unafanywa kutokana na mahitaji na kuongeza kuwa watakapofikia mahitaji hayo, watapunguza uzalishaji na kupunguza urutubishaji hadi kufikia asilimia 3.5.

Lakini haikuwa wazi kama matamshi hayo ya Abbas ndiyo yatakuwa msimamo rasmi wa Iran wakati wa mazungumzo haya ya Mjini Istanbul yanayofanyika miezi kumi na minne tangu kuvunjika kwa mazungumzo yaliyopita.

Matumaini ya kufikia muafaka
Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya Nje wa Iran, Ali Akbar Saleh, alinukuliwa na tovuti ya Bunge la Iran akielezea matumaini yake ya kuwepo na mufaka katika mazungumzo hayo, lakini akaonya kuwa nchi yake haitakubali masharti yoyote kabla ya kuhudhuria mkutano huo.

Kituo cha Nantaz kama kilivyoonyeshwa na picha ya SetilaitiPicha: AP

Iran inasisitiza kuwa chini ya Mkataba wa kuzuia kuenea kwa silaha za atomik, ina haki ya kurutubisha nishati ya uranium ili kuzalisha mafuta na inasema kuwa inatafuta viwango vya urutubishaji vitakavowezesha vinu vyake kwa ajili ya utafiti na kuzalisha umeme.

Baada ya kutolewa tangazo la Iran kurudi katika meza ya mazungumzo kuhusu mpango wake huu, bei za mafuta katika soko la dunia zilipungua kwa zaidi ya dola moja.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga\APE\RTRE
Mhariri: Mohamed Abdul Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW