Iran yalaani hatua ya kurejeshewa vikwazo na UN
28 Septemba 2025
Matangazo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema katika taarifa yake kwamba itatetea kwa uthabiti haki na maslahi yake ya kitaifa na kwamba hatua yoyote ya kukiuka haki na maslahi ya watu wake itakabiliana na majibu makali na kuongeza kwamba uamuzi huo hauna msingi wa kisheria ikiyataka mataifa kutoutambua uamuzi huo ilioutaja si halali.
Vikwazo hivyo vya vya Umoja wa mataifa vimeipiga marufuku Iran kuendeleza shughuli zinazohusiana na nyuklia na makombora ya masafa marefu, vimeanza kutumia kuanzia leo Jumapili. Hata hivyo mataifa ya Magharibi yamesisitiza kuwa bado meza ya mazungumzo iwa wazi.