1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yamkamata naibu mhariri wa shirika la habari la Fars

6 Desemba 2022

Naibu mhariri mkuu wa shirika la habari la Fars nchini Iran amekamatwa na mamlaka za serikali wiki moja baada ya shirika hilo kuripotiwa kukumbwa na shambulizi la mtandaoni

Iran | Nachrichtenagentur Fars wurde gehackt
Picha: Iranisch

Shirika la habari la taifa IRIB limetangaza taarifa hiyo jana usiku likisema Abbas Darvish Tavanger amekamatwa kwa kutowa taarifa za upotoshaji na ataendelea kushikiliwa wakati uchunguzi unafanyika.

Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao wake wa Telegram shirika hilo la Fars lilisema mnamo Novemba 26 kwamba shughuli zake zimeingiliwa na wadukuzi wa mtandao.

Baadaye kundi linalojiita Black Reward lilidai kuhusika na shambulio hilo la mtandao na kusema limefanikiwa kupata nyaraka chungunzima za siri.

Kukamatwa kwa naibu mhariri mkuu wa Fars kumekuja wakati Iran ikikabiliwa na machafuko yaliyosababishwa na tukio la kifo cha msichana wa miaka 22 Mahsa Amini mikononi mwa polisi.