1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yamnyonga mtu mmoja tangu kuzuka maandamano

8 Desemba 2022

Mahakama nchini Iran imesema mtu mmoja aliyekuwa amefunguliwa mashtaka ya kumjeruhi mwanajeshi wakati wa maandamano yanayoendelea nchini humo amenyongwa.

Symbolbild Iran Hinrichtung
Picha: Marius Becker/dpa/picture alliance

Hii ni hukumu ya kwanza ya mauaji kutolewa na mahakama hiyo katika kipindi cha miezi mitatu ya maandamano.

Ujumbe ulioandikwa kwenye tovuti ya idara ya mahakama ya Mizan umesema, Mohsen Shekari, mwandamanaji aliyefunga barabara ya Sattar Khan mjini Tehran mnamo Septemba 25 na kumjeruhi afisa mmoja wa ulinzi kwa panga, amenyongwa.

Mahakama hiyo imesema Shekari amepatikana na hatia ya kupigana na kutoa silaha kwa lengo la kuuwa, kufanya ugaii na kutatiza utulivu na usalama wa jamii.

Mahakama nyengine ya Iran hapo juzi Jumanne iliwahukumu watu wengine watano kinyongo kwa kumuua mwanajeshi wa jeshi lenye nguvu la mapinduzi nchini humo. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW