1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yaomboleza kifo cha kamanda wa walinzi wa mapinduzi

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika mjini Tehran kuhudhuria mazishi ya Kamanda mwandamizi wa Kikosi cha ulinzi wa Mapinduzi IRGC, Razi Moussavi, aliyeuawa katika kile ambacho Iran imesema ni shambulizi la Israel.

Iran | Seyed Razi Mousavi wa IRGC
Kamanda mwandamizi wa Kikosi cha ulinzi wa Mapinduzi, IRGC, Razi Moussavi,Picha: Tasnim News Agency via ZUMA Press Wire/picture alliance

Mkuu wa kikosi cha IRGC Hossein Salami amemsifu Moussavi kama mmoja wa makamanda wenye uzoefu na ufanisi zaidi katika mhimili wa upinzani - akimaanisha makundi ya wapiganaji wenye mafungamano na Tehran katika kanda ya Mashariki ya Kati. 

Msemaji wa IRGC Ramezan Sharif alionya jana kuwa majibu yao kwa mauaji ya Moussavi yatakuwa mchanganyiko wa hatua za moja kwa moja pamoja na nyingine zinazoongozwa na mhimili wa upinzani.

Sharif amedai kuwa mauaji ya Moussavi yalitokana na kushindwa kwa jeshi la Israel kuzuwia uvamizi wa Hamas wa Oktoba 7.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW