1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yaondoa uwezekano wa kuzungumza na Marekani kwa sasa

1 Julai 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi jana Jumatatu alifutilia mbali uwezekano wa kurejea kwenye mazungumzo na Marekani hivi karibuni na kusema Tehran inataka kuhakikishiwa kwamba haitashambuliwa tena.

Ureno Lisbon 2024 | Abbas Araghchi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi akizungumza na waandishi wa habari 27.11.2024Picha: Horacio Villalobos/Corbis/Getty Images

Araghchi alisema hayo kwenye mahojiano na kituo cha CBS Evening News cha Marekani, alipoulizwa kuhusu matamshi ya Rais Donald Trump kwamba mazungumzo ya nyuklia na Iran yanaweza kuanza tena mapema wiki hii.

Pamoja na hakikisho hilo, Araghchi amesema bado wanahitaji muda zaidi, ingawa milango ya diplomasia kamwe haitafungwa.

Marekani na Iran zilikuwa katika mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran wakati Israel iliposhambulia maeneo ya nyuklia ya Iran na miundombinu ya kijeshi, huku Marekani ikijiunga kwa kulipua maeneo matatu ya nyuklia ya Fordo, Natanz na Isfahan, mnamo Juni 21.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW