1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yaonya azimio la nchi tatu za Ulaya ndani ya IAEA

20 Novemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran ameyaonyao mataifa matatu ya Ulaya dhidi ya kushinikiza kupitishwa azimio la kuikosoa Iran kwenye mkutano wa Shirika la IAEA unaoanza leo Jumatano mjini Vienna.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran Abbas Araghchi
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran Abbas Araghchi Picha: Marwan Naamani/picture alliance/dpa

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran Abbas Araghchi ameyaonya leo mataifa matatu ya Ulaya dhidi ya kushinikiza kupitishwa azimio la kuikosoa Iran kwenye mkutano wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki IAEA unaoanza leo Jumatano mjini Vienna.

Akizungumza na waziri mwenzake wa Ufaransa, Araghchi, amesema Iran inakosoa kwa matamshi makali uamuzi wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza wa kuwasilisha rasimu ya azimio hilo linalolenga kuongeza mbinyo kwa Tehran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.

Soma pia: Grossi akutana na viongozi wa Iran mjini Tehran 

Nchi hizo tatu zinataka kuilazimisha Iran kuanza tena kutekeleza kikamilifu kanuni za usalama wa nishati ya atomiki na kuondoa mashaka yote ya muda mrefu ya shirika la IAEA juu ya mradi wake wa nyuklia.

Mkuu wa IAEA, Rafael Grossi aliitembea Iran mapema mwezi huu ikiwa ni pamoja na kuvizuru vituo viwili vya urutubishaji madini ya urani katika safari ambayo Tehran ilisema imefungua njia ya mashauriano chanya kati ya pande hizo mbili.

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW