1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaonya dhidi ya vitisho vya mataifa ya kigeni

7 Januari 2026

Jamhuri ya kiislamu ya Iran imeonya dhidi ya vitisho vya mataifa ya kigeni, ikisema haitokaa kimya kuacha iendelee kuchokozwa,baada ya Israel na Marekani kuunga mkono maandamano ya wananchi Iran

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa kwenye msuguano wa jadi na Marekani na Israel
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa kwenye uhasama wa jadi na Marekani na IsraelPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Mkuu wa majeshi wa Iran Jenerali Amir Hatami ametowa onyo kwamba nchi yake haitokaa kimya na kuruhusu kutolewa vitisho na mataifa ya kigeni yenye nguvu, baada ya Marekani na Israel kutangaza kuyaunga mkono maandamano ya kuipinga serikali ya Tehran. 

Mahakama ya Iran yaapa kuwakabili vikali waandamanaji

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Jenerali Hatami, amesema Jamhuri hiyo ya Kiislamu ya Iran inayatazama matamshi ya uchochezi na kichokozi dhidi ya taifa hilo kuwa vitisho na Tehran haitoruhusu kuyaacha yaendelee bila kujibiwa.

Hivi karibuni rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuingilia kati mzozo wa Iran ikiwa waandamanaji watauwawa, huku waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akitangaza kuyaunga mkono maandamano hayo 

Mzozo wa Israel na Iran.

Wakati huohuo, Iran pia imemyonga mwanamme mmoja aliyekutwa na hatia ya kuendesha vitendo vya ujasusi ndani ya Iran kwa niaba ya shirika la Ujasusi la Israel, Mossad.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW