1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iran yaonya hatari ya mabomu Mlango Bahari wa Hormuz

9 Aprili 2026

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran limeonya kuhusu mabomu yaliyotegwa kwenye maji katika Mlango Bahari wa Hormuz, hali inayokwamishwa juhudi za kuufungua, baada ya makubaliano ya kusitisha vita na Marekani.

Bandari ya Abbas, Iran | Mlango Bahari wa Hormuz 10.12.2023
Bandari ya Abbas ya nchini Iran iliyo kwenye Mlango Bahari wa HormuzPicha: REUTERS

Jeshi la wanamaji la Iran limechapisha ramani inayoonesha eneo hatari katika Mlango Bahari wa Hormuz hasa sehemu zinakopita meli za biashara. Hayo yanajiri wakati Iran ikitishia kuwa itarejea kwenye mapigano kutokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon.

Utata wazidi uhusika wa Lebanon kwenye makubaliano ya kusitisha vita

Tehran inasisitiza kuwa kusimamisha mashambulizi Lebanon ni sehemu ya makubaliano ya kusitisha vita wakati Israel na Marekani zikipinga hilo.

Wakati huohuo wawakilishi  wa Iran wanatarajiwa kuwasili mjini Islamabad baadaye leo kwa ajili ya mazungumzo ya usuluhishi na Marekani yanayosimamiwa na Pakistan.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW