1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yarusha setilaiti kama sehemu ya mpango wake wa nyuklia

20 Januari 2024

Iran imesema leo kuwa imerusha setilaiti aina ya Sorayya katika mzingo wa dunia, hatua ya hivi karibuni ambayo mataifa ya Magharibi yanahofia kuwa itaboresha uwezo wake wa nyuklia.

Satelaiti aina ya Galileo
Satelaiti aina ya GalileoPicha: picture-alliance/dpa

Tangazo hilo, lililotolewa kupitia runinga ya taifa, limeeleza kuwa urushaji huo wa setilaiti ni sehemu ya mpango wake wa anga wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu wa Iran.

Awali, Marekani iliwahi kusema kuwa urushaji wa satelaiti ya Iran unakwenda kinyume na azimio la Baraza la Usalama na kuitaka nchi hiyo kutojihusisha na shughuli zozote za kurutubisha madini ya Uranium na hivyo kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia.

Vikwazo vya Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran vilikamilika mwezi Oktoba mwaka uliopita. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW