Iran yasema haiiamini Marekani
1 Juni 2026
Akizungumza kupitia ujumbe kwa njia ya video uliorushwa na televisheni ya taifa siku ya Jumapili (Mei 31), Mohammad Bagher Ghalibaf, alisema timu yake itahakikisha masuala muhimu yenye maslahi kwa watu wa Iran yanazingatiwa kabla ya kusaini makubaliano yoyote na Marekani.
Kauli hiyo ya spika wa bunge la Iran ilitolewa masaa machache baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba Rais Donald Trump wa Marekani amerejesha pendekezo la mkataba wa amani kwa Iran, wenye masharti na msimamo mkali zaidi, hali inayoashiria kina cha tafauti kubwa zilizopo kati ya pande hizo mbili.
Utata wowote uliomo kwenye pendekezo hilo huenda ukachelewesha kukomeshwa rasmi kwa vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran miezi mitatu iliyopita na pia kufunguliwa tena kwa Mlango Bahari wa Hormuz, ambao Tehran imeufunga kwa sababu za kiusalama tangu kuanza kwa vita hivyo - na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani.