1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema haijarejea kikamalifu kwenye ushirikiano na IAEA

27 Agosti 2025

Iran imesema leo kwamba kurejea kwa wakaguzi wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa hakumaanishi kuanza tena kikamilifu kwa ushirikiano na IAEA .

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na spika wa bunge la Lebanon Nabih Berri mjini Beirut mnamo Juni 3, 2025
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas AraghchiPicha: Marwan Naamani/ZUMA Press/IMAGO

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amenukuliwa na televisheni ya taifa akisema hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa kuhusu mfumo mpya wa ushirkiano na Shirika la Kudhibiti Nguvu za Atomiki duniani, IAEA na kwamba bado wanabadilishana maoni.

Mazungumzo ya nyuklia ya Iran yakamilika bila mafanikio

Kwa upande wake, msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, Behrouz Kamalvandi, amesema wakaguzi hao wa IAEA watasimamia ubadilishaji wa mafuta katika kinu cha nyukliacha Bushehr kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Hata hivyo, hakusema kama wakaguzi hao wataruhusiwa kufika maeneo mengine ya vinu vya nyuklia, ikiwa ni pamoja na Fordo na Natanz, ambavyo vililengwa wakati wa vita.

Kurejea kwa wakaguzi hao kumekuja baada ya wanadiplomasia wa Irankufanya mazungumzo na wenzao kutoka Uingereza, Ufaransa na Ujerumani hapo jana mjini Geneva.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW