1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iran yasema haitosita kujibu mashambulio dhidi yake

5 Februari 2024

Iran imesema haitosita kujibu mashambulizi yoyote yatakayofanywa dhidi ya ardhi yake, baada ya Marekani kushindwa kusema waziwazi ikiwa imeondoa uwezekano wa kuishambulia Iran.

Iran, Tehran | Ebrahim Raisi
Rais wa Iran Ebrahim RaisiPicha: Rouzbeh Fouladi/ZUMA/picture alliance

Iran imesema haitosita kujibu mashambulizi yoyote yatakayofanywa dhidi ya ardhi yake, baada ya Marekani kushindwa kusema waziwazi ikiwa imeondoa uwezekano wa kuishambulia Iran.

Siku ya Jumapili mshauri wa masuala ya usalama katika ikulu ya White House, Jake Sullivan alisema Marekani itaendelea kuyashambulia makundi yanayoungwa mkono na Iran katika nchi za Iraq na Syria.

Na kwa upande wake Iran kupitia msemaji wa wizara yake ya mambo ya nje Nasser Kanani imeijibu Marekani leo Jumatatu kwa kusema Jamhuri hiyo ya kiislamu mara zote imeonesha inachukuwa hatua kujibu  kitisho chochote cha usalama kinachoikabili.Iran pia imelaani mashambulio ya nchi za Magharibi dhidi ya Yemen,Syria na Iraq.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW